13, wanaodaiwa kutuma SMS za 'ile hela tuma kwenye Namba hii' wapandishwa kizimbani. - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

13, wanaodaiwa kutuma SMS za 'ile hela tuma kwenye Namba hii' wapandishwa kizimbani.


Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.

Vijana 13 wanaodaiwa kutuma sms kwa watu tofauti tofauti wamefikishwa katika mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka matano likiwemo la utakatishaji wa fedha wa zaidi ya milioni 154.

Washtakiwa hao wameshtakiwa chini ya sheria ya uhujumu uchumi.

Wakisomewa mashtaka yao kwenye kesi hiyo namba 58 ya 2018 leo Agosti 7.2018 mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Kelvin Mhina, Wakili wa Serikali Mkuu,Tumaini Kweka alidai washtakiwa hao wanakabiliwa na shtaka la kula njama, kuchapisha taarifa za uongo, mashtaka mawili ya kusambaza na shtaka moja la utakatishaji wa fedha.

Wakili, Kweka amewataja washtakiwa hao kuwa ni Boniface Maombe, David Luvanda, Moshi Sungura, Amos Bosco, Lule Kadenge, Jofrey Kapangamwaka, William Nturo, Regius Mauka, Collins Mwang'omolan Francis Kapalata, Kasonde Kapela, Enock Mwandaji na Pascal Kiatu.

Akisoma hati ya mashtaka wakili wa serikali Mwandamizi Nasoro Katuga amedai kati ya Machi 6 na Juni 2018, washta... Continue reading ->Source: Issa MichuziRead More