3,955 WAENDELEA KUNUFAIKA NA MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASKINI - TASAF SHINYANGA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

3,955 WAENDELEA KUNUFAIKA NA MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASKINI - TASAF SHINYANGA

Jumla ya walengwa 3,955 wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini unaotekelezwa na Serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii –TASAF wanaendelea kunufaika na mpango huo katika Manispaa ya Shinyanga.
Hayo yamebainishwa jana Agosti 9,2018 na Mratibu wa Kunusuru Kaya Maskini - TASAF Manispaa ya Shinyanga Octavina Kiwone akizungumza na waandishi wa habari.
Kiwone alisema Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini katika manispaa ya Shinyanga ulianza kutekelezwa mwaka 2015 ukiwa na walengwa 4,244 ambao hata hivyo walipungua kutokana na wengine kufariki na wengine tuliwaondoa kwa kukosa sifa za kuwa kwenye mpango lakini mpaka sasa tuna walengwa 3,955,
"Tangu mwaka 2015 mpaka sasa tumepokea fedha za serikali jumla ya shilingi bilioni 3,fedha ambazo tumewapa walengwa ni shilingi bilioni 2.7 na tayari zimewafikia walengwa ambapo fedha hizi zinawasaidia kwa sababu wanapewa fedha kisha kufundishwa namna ya kutumia fedha hizo",alifafanua.Mratibu wa Kunusuru Kaya Maskini - TASAF Manispaa ya Shinyanga Octavina Kiwon... Continue reading ->Source: Issa MichuziRead More