52% YA WATANZANIA WAMEPIMA VVU-SERIKALI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

52% YA WATANZANIA WAMEPIMA VVU-SERIKALI


Na WAMJW-DOM
SERIKALI imesema kuwa Watanzania wapatao 2,405,296 hadi kufikia tarehe Oktoba 2018 walipima VVU kupitia Kampeni ya ‘Furaha Yangu’ ambao ni sawa na asilimia 52 ya lengo la kuwapima watanzania wapatao 4,638,639 hadi Desemba 2018.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile katika kikao cha kamati ya bunge ya huduma za jamii kilichofanyika leo jijini Dodoma.
“Hadi kufikia tarehe 31 Oktoba 2018, jumla ya watanzania 2,405,296 walikuwa wamepima VVU kupitia Kampeni ya ‘Furaha Yangu’ ambao ni sawa na asilimia 52 ya lengo la kuwapima watanzania wapatao 4,638,639 hadi Desemba 2018” Alisema Dkt. Ndugulile
Dkt. Ndugulile aliendelea kusema kuwa Miongoni mwa wote waliopima, wanaume walikuwa ni asilimia 44 huku wanawake wakiwa ni asilimia 56. Kati yao, watu 70,436 (2.9%) walikutwa na maambukizi ya VVU, ambapo wanaume 27,984 (2.6%) na wanawake ni 42,452 (3.2%).
Aidha, Dkt. Ndugulile alisema kuwa Wizara kwa kushirikiana... Continue reading ->

Source: Issa MichuziRead More