Aaron Ramsey awaaga rasmi Arsenal, Juventus wamkaribisha kwa madaha, hiki ndio kitita atakachokuwa akipokea - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Aaron Ramsey awaaga rasmi Arsenal, Juventus wamkaribisha kwa madaha, hiki ndio kitita atakachokuwa akipokea

Kiungo wa kati wa Arsenal Aaron Ramsey ametia saini makubaliano ya awali ya kujiunga na klabu ya Juventus msimu ujao kwa katika cha pauni £400,000 kwa wiki. Nyota huyo wa miaka 28 amekubali mkataba wa miaka minne utakaomwezesha kujiunga na ligi ya champions ya Italia bila malipo baada ya kuwa Arsenal kwa miaka 11.

Ramsey alifuzu sehemu ya kwanza ya uchunguzi wa kimatibabu mwezi Januari, na kuchagua Juve baada ya kushauriana na wadau kadhaa wa klabu hiyo.

Atakuwa mchezaji wa Uingereza anayelipwa mshahara mkubwa.

Mkataba wa mchezaji huyo wa kimataifa wa Wales unakamilika Juni 30 na Gunners hawatapokea malipo yoyote atakapo ondoka.

Ikithibitisha mpango huo, Juventus imesema italipa ada ya pauni milioni £3.2 lakini haikuelezea ada hiyo ni ya nini.

Arsenal imesema mchango wa Ramsey ulikuwa mkubwa sana katika klabu hiyo na kuongeza kuwa “atakasalia katika kumbu kumbu ya historia” ya mashabiki.

Akiandika katika mtandao wake Instagram, Ramsey aliwashukuru mashabiki wa A... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More