ABDALLA SHAIBU 'NINJA', TINOCO WASIMAMISHWA MECHI TATU - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

ABDALLA SHAIBU 'NINJA', TINOCO WASIMAMISHWA MECHI TATU

Na Zainab Nyamka, Globu ya JamiiSHIRIISHO la mpira wa miguu nchini (TFF) kupitia Kamati ya Nidhamu ya TFF imetoa hukumu baada ya kuwatia hatiani wachezaji wa Abdallah Shaibu na Benedict Tinoco kwa kuwakuta na hatia ya kutenda makosa ya utovu wa nidhamu.
Kamati ya nidhamu imemkuta na hatia Ninja kwa kosa la kumpiga kiwiko mchezaji wa timu ya Coastal Union kwenye mchezo wa ligi kuu (TPL) na Kamati imempa adhabu ya kufungiwa kutocheza mechi tatu mfululizo/zinazofuatana kwa mujibu wa kifungu cha 48(1)(d) cha Kanuni za Nidhamu TFF.
Katika maamuzi mengine Kamati ya nidhamu ya Nidhamu ya TFF, imemtia hatiani Mchezaji wa Mtibwa Sugar Benedict Mlekwa Tinoco kwa kosa la kumkanyaga kwa makusudi mchezaji wa timu Biashara United Fc aliyekuwa ameanguka baada ya kuchezewa rafu, Kamati imempa adhabu ya kufungiwa kutocheza mechi tatu mfululizo/zinazofuatana kwa mujibu wa kifungu cha 48(1)(d) cha Kanuni za Nidhamu TFF.
Mbali na hilo, Kamati pia imetoa maamuzi kwenye mashauri mengine kwa Simba na Yanga wot... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More