ABDI BANDA: SASA NAWEZA KUCHEZA POPOTE DUNIANI, SUALA LA MUDA TU - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

ABDI BANDA: SASA NAWEZA KUCHEZA POPOTE DUNIANI, SUALA LA MUDA TU

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
BEKI wa kimataifa wa Tanzania, Abdi Hassan Banda amesema kwamba kwa uwezo wake hivi sasa anajiona anaweza kucheza popote.
Akizungumza kwa simu jana kutoka Afrika Kusini baada ya kuiongoza timu yake, Baroka FC kutoa sare ya 1-1 na Kaizer Chiefs juzi katika mchezo wa Ligi Kuu, Banda amesema kwamba kwa uwezo wake wa sasa anaweza kucheza poote duniani.
“Uwezo wangu umepanda sana ndani ya wastani wa mwaka mmoja wa kucheza Afrika Kusini, naamini kabisa kwa sasa ninaweza kucheza sehemu yoyote duniani. Ni suala la kusubiri muda tu bahati itokee nipate timu yenye maslahi makubwa kuliko hapa,”amesema Banda.

Abdi Banda amesema kwa sasa anajiona anaweza kucheza popote duniani

Katika mchezo wa juzi Uwanja wa Peter Mokaba mjini Polokwane, Petersburg, beki Daniel Cardoso alianza kujifunga dakika ya 36 kuwapatia Baroka FC la kuongoza, kabla ya mkongwe Siphiwe Tshabalala kuisawazishia Kaizer dakika ya 43.  
Matokeo hayo yanaifanya Baroka FC ifikishe pointi nne baada ya ... Continue reading ->Source: Bin ZuberyRead More