Abdul Nondo ile kesi yake ya kujiteka, aachiwa huru na Mahakama ya Mkoa wa Iringa - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Abdul Nondo ile kesi yake ya kujiteka, aachiwa huru na Mahakama ya Mkoa wa Iringa

Mahakama ya Mkoa wa Iringa leo Novemba 05, 2018 imemuachia huru aliyekuwa Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi (TSNP), Abdul Nondo.


Image result for abdul nondoAbdul Nondo

Mnamo mwezi Agosti 27 mwaka huu, Mahakama hiyo ilimkuta Nondo na kesi ya kujibu kwa mashtaka ya kusambaza taarifa za uongo akidai kutekwa, huku ikimtaka alete mashahidi watano kwenye utetezi wake.


Abdul Nondo alikuwa anakibiliwa na kesi ya kutoa taarifa za uongo kuwa alitekwa na watu wasiojulikana mapema mwanzoni mwa mwaka huu.


Nondo ambaye pia alikuwa mwanafunzi wa mwaka wa tatu katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), kabla hajasimamishwa masomo kutokana na kesi hiyo, alidaiwa pia kutoa taarifa za uongo kwa polisi katika Kituo cha Mafinga mkoani Iringa.


The post Abdul Nondo ile kesi yake ya kujiteka, aachiwa huru na Mahakama ya Mkoa wa Iringa appeared first on Bongo5.com.... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More