Acacia Yachafuka kwa Tuhuma za Rushwa - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Acacia Yachafuka kwa Tuhuma za Rushwa

Kampuni ya uchimbaji wa madini ya Acacia, kupitia kampuni yake ya North Mara Gold Mine iliyopo mkoani Mara, imeingia katika kashfa baada ya Maafisa Waandamizi wa kampuni hiyo wawili kushtakiwa kwa tuhuma za rushwa ili kupata upendeleo dhidi ya maslahi ya wanavijiji na Serikali ya mkoa huo.
Washtakiwa wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Wilaya ya Tarime siku ya Jumatato Oktoba 10, 2018 na kusomewa mashtaka ya rushwa chini ya Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na. 11 ya Mwaka 2007.
Kwa nyakati tofauti, watuhumiwa Marteen Van Der, Johannes Jensen, Joseph Kleruu, Bomboga Chikachake, Tanzania O’mtima na Abel Kinyimari wameshtakiwa kwa utoaji na upokeaji wa rushwa wa namna mbalimbali kwa Maafisa wa Serikali na wanasiasa wa mkoani Mara.
Mei 17, 2013 watuhumiwa Marteen Van Der na Johannes Jensen walitoa rushwa ya jumla ya shilingi 93,896,000 kwa Mthamini Mkuu wa Ardhi wa Serikali Adam Yusuph pamoja na kumpa Peter Mrema 30,000,000 ili kupata upendeleo wakati wa upimaji wa ardhi kwa aji... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More