ADA ZA SHULE NA BODABODA KUTOLEWA KWA MARA YA KWANZA KUPITIA MWALIMU COMMERCIAL BANK - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

ADA ZA SHULE NA BODABODA KUTOLEWA KWA MARA YA KWANZA KUPITIA MWALIMU COMMERCIAL BANK

Na Leandra Gabriel, Blogu ya JamiiMWALIMU Commercial Bank imefanya droo yake ya kwanza ya kampeni ya "Weka Akiba na Ushinde"  iliyoanza rasmi Septemba 10 mwaka huu na itaendelea mpaka Novemba 30 mwaka huu, na hiyo ikiwa na moja ya mikakati ilinayofanywa na benki hiyo hasa katika kutoa hamasa kwa wateja wao katika kujiwekea akiba.
Akizungumza na vyombo vya habari Mkurugenzi Mkuu wa  Mwalimu Commercial Bank (MCB,) Ronald Manongi  amesema kuwa mteja akijiwekea akiba katika akaunti yake kuanzia shilingi 30,000 na kuendelea wakati wote wa kampeni hiyo  basi atapata tiketi moja ya kuingia katika droo inafanyika kila mwezi.
"Mteja anapoweka akiba zaidi hupata nafasi zaidi na kupata tiketi nyingi zaidi na kujiweka katika nafasi ya ushindi zaidi katika droo kubwa na zawadi zitakazotolewa ni pamoja na  ada za shule na bodaboda." ameeleza Manongi.
Aidha Manongi amesema kuwa Mwalimu Commercial Bank imeanzisha akaunti ya tukutane Januari ambayo inamuwezesha mteja kujiwekea akiba kidogo kidogo ili awe... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More