AFREXIMBANK KUIPATIA TANZANIA ZAIDI YA SH. TRILIONI MOJA KUGHARAMIA UJENZI WA RELI NA VITUO VYA BIASHARA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

AFREXIMBANK KUIPATIA TANZANIA ZAIDI YA SH. TRILIONI MOJA KUGHARAMIA UJENZI WA RELI NA VITUO VYA BIASHARA

Na: WFM,  Mjini Bali IndonesiaAfrican Export Import Bank (Afreximbank) ya Misri, imeonyesha nia ya kuipatia Tanzania mkopo wa zaidi ya Shilingi trilioni moja (dola za Marekani zaidi ya milioni 500) kwa ajili ya kutekeleza miradi ya kipaumbele hasa ya miundombinu ya reli na kujenga vituo vya biashara (SEZ and Industrial parks). Hayo yalibainishwa mjini Bali Indonesia, na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isdor Mpango baada ya Mkutano na Makamu wa Rais wa Afreximbank Bw. Amr Kamel,  uliofanyika  wakati wa mikutano ya mwaka  ya Benki ya Dunia (WB) na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) ikiendelea.Waziri Mpango, alisema kuwa Afreximbank imethibitisha kuwa ipo tayari kutoa mkopo wa  dola za Marekani milioni 125  (takribani Shilingi bilioni 285.9) kwa ajili ya ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha Kimataifa  (SGR),  kipande cha Morogoro hadi Makutupora mkoani Dodoma. “Afreximbank wanania pia ya kutoa  dola milioni 400 (takribani Sh. Bilioni 914.9) ambazo wanaweza kut... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More