African Lyon kuikimbia Dar - Shaffih Dauda | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

African Lyon kuikimbia Dar

Mmiliki wa klabu ya African Lyon Rahim Zamunda Kangezi anapambana kuihamisha timu hiyo kutoka Dar es Salaam kwenda mkoa mwingine kwa sababu ya kukosa mashabiki wa kuiunga katika jiji la Dar.


“Huwezi kuwa na timu yatima, aliyeianzisha timu alikosea, umewahi kusikia timu haina mashabiki? Sio rahisi kuendesha timu bila mashabiki ndio maana tunataka tuhame Dar es Salaam.”


“Kuna mikoa mitatu tunaongea nayo lakini tutaona ni mkoa gani halafu tutahama moja kwa moja hatuendi kwa ajili ya michezo ya ligi. Tukiondoka hatutarudi tena, tunataka tuwe na mji wetu, Dar ni pagumu sana Simba na Yanga wameshachukua mji.”


“Siwakimbii Simba na Yanga lakini inabidi ujue maana ya ‘African Lyon’ Africa ni Yanga Afrika, Lyon ni Simba kwa hiyo walikuwa wanataka tuunganishe mashabiki tukae katikati lakini mpango huo haukufanikiwa.”


Chanzo @ufmradiotz


Source: Shaffih DaudaRead More