AFRICAN LYON YAKAMILISHA MECHI NNE BILA USHINDI, COASTAL UNION YAOKOTA POINTI YA SITA - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

AFRICAN LYON YAKAMILISHA MECHI NNE BILA USHINDI, COASTAL UNION YAOKOTA POINTI YA SITA

Na Sada Salmin, DAR ES SALAAM
TIMU ya African Lyon leo imekamilisha mechi nne bila ushindi, baada ya kulazimishwa sare ya bila kufungana na Coastal Union ya Tanga katika mchezo wa Ligi Kuu Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam.
Sare hiyo inayokuja baada ya kufungwa mechi moja na kutoa sare mbili awali, inawafanya wajiongezee pointi moja na kufikisha tatu, wakati wapinzani wao, Coastal Union wanafikisha pointi sita katika mechi ya nne, awali wakishinda moja na kutoa sare mbili.  
Coastal Union walicheza vizuri zaidi kipindi cha kwanza na kutengeneza nafasi nzuri, lakini bahati mbaya wakashindwa kuzitumia ikiwemo ya dakika ya 25 pale washambuliaji waliposhindwa kumalizia krosi nzuri ya Hamisi Mustafa.

Mshambuliaji wa Coastal Union, Hajji Ugando akimiliki mpira mbele ya beki wa African Lyon leo mjini Dar es Salaam

Mashambulizi ya kusisimua ya African Lyon yote yalifanywa na mkongwe Haruna Moshi ‘Boban’ dakika ya 28 akipiga nje kidogo ya lango na dakika ya 39 akipiga shuti lililodakwa na ki... Continue reading ->


Source: Bin ZuberyRead More