AGAPE YAENDESHA BONANZA LA MICHEZO KUTOA ELIMU YA AFYA YA UZAZI NA UJINSIA VIJIJINI - Kajunason | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

AGAPE YAENDESHA BONANZA LA MICHEZO KUTOA ELIMU YA AFYA YA UZAZI NA UJINSIA VIJIJINI

Shirika lisilo la kiserikali AGAPE AIDS CONTROL PROGRAM la Mkoani Shinyanga linalojishughulisha na masuala ya jamii, limetoa elimu ya afya ya uzazi na ujinsia kwa njia ya bonanza la michezo kwenye vitongoji vya Buchamike,Shabuluba, Mwagala na Uswahilini vilivyopo pembezoni mwa kata ya Usanda Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.

Bonanza hilo limeendeshwa Ijumaa Mei 10, 2019 kwenye viwanja vya michezo vya kitongoji cha Buchambi kata ya Usanda ambapo kumefanyika michezo mbalimbali ikiwemo kukimbiza kuku, mbio za baiskeli pamoja na mpira wa miguu na washindi wamezawadiwa zawadi mbalimbali ikiwamo kupewa kuku pamoja na mbuzi.

Akizungumza kwenye bonanza hilo Mratibu wa mradi  wa afya ya uzazi na ujinsia kutoka Shirika hilo la Agape Lucy Maganga, amesema wameamua kutoa elimu hiyo kwa njia ya michezo ili kufikisha elimu kwa wananchi, kuachana na masuala kupenda kuozesha wanafunzi ndoa za utotoni, pamoja na kuwapatia ujauzito na hatimaye kuacha masomo yao.

Alisema Shirika hilo limekuwa likiend... Continue reading ->Source: KajunasonRead More