AGAPE YAKUTANA NA VIONGOZI WA JAMII USANDA KUTOKOMEZA MILA NA DESTURI ZINAZOKANDAMIZA WATOTO - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

AGAPE YAKUTANA NA VIONGOZI WA JAMII USANDA KUTOKOMEZA MILA NA DESTURI ZINAZOKANDAMIZA WATOTOAfisa Ustawi wa Jamii Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Elizabeth Mweyo akizungumza katika kikao cha Viongozi wa Jamii kata ya Usanda.

Shirika la Agape AIDS Control Program la Mkoani Shinyanga limekutana na viongozi wa jamii katika kata ya Usanda halmashauri ya wilaya ya Shinyanga kwa ajili ya kutambua na kutokomeza mila na desturi kandamizi zinazochangia ukatili dhidi ya wanawake na watoto ili kupunguza mimba na ndoa za utotoni na maambukizi ya VVU na UKIMWI.
Kikao hicho cha siku moja kimefanyika leo Jumanne Machi 19,2019 katika shule ya msingi Shingida iliyopo katika kata ya Usanda na kukutanisha pamoja wenyeviti wa vitongoji 30 vya kata hiyo,viongozi wa kimila,dini,watu wenye ulemavu na vijana. 
Akizungumza wakati wa kikao hicho, Afisa mradi wa afya ya uzazi na ujinsia kwa vijana kutoka Shirika la Agape, Lucy Maganga alisema viongozi wa jamii wanayo nafasi kubwa ya kuielimisha jamii kuachana na mila na desturi kandamizi ambazo zimekuwa zikichangia mimba na ndoa za utotoni. 
“Mila ... Continue reading ->
Source: Issa MichuziRead More