AGIZO LA RAIS MAGUFULI LAANZA KUTEKELEZWA KYAKA MISSENYI. - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

AGIZO LA RAIS MAGUFULI LAANZA KUTEKELEZWA KYAKA MISSENYI.

Anaandika Abdullatif Yunus wa Michuzi TV.
Siku moja baada ya Rais John Pombe Magufuli kuagiza kushugulikiwa kero ya Maji kwa wakazi wa Kyaka, Kata Burifani, na Kata jirani, katika Wilaya ya Missenyi, Waziri wa Maji Professa Makame Mbarawa amefika Wilayani humo ili kuanza utekelezaji wa agizo hilo.
Akiambatana na Safu ya wataalam mbalimbali wa Maji kutoka BUWASA na wengine kutoka Mwanza pamoja na Wizarani, amefika eneo la Kyaka na kufanya Mkutano wa hadhara ambapo katika mkutano huo ameahidi kuanza kutekeleza agizo la Mhe. Rais kwa haraka ili kutatua kero hiyo ndani ya miezi mitano.
Aidha Professa Mbarawa amesema kuwa kwa sasa Wizara ya Maji imejipanga vyema kuhakikisha miradi ya Maji inatekelezwa na Wakandarasi wenye sifa na uwezo kwani kipindi cha nyuma miradi mingi ilikwama kutokana na Kandarasi wabovu, na kukiri kuwa uwepo wa ukiritimba na urasimu, ambapo watumishi wachache wasiokuwa waadilifu wamekuwa wakishirikana na wakandarasi wabovu kutekeleza miradi ya Maji isiyokuwa na Viwango, ... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More