Agizo La Waziri Lugola Kwa Wananchi Ambao Hawajapata Kitambulisho Cha Taifa Nchini - Mwanaharakati Mzalendo | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Agizo La Waziri Lugola Kwa Wananchi Ambao Hawajapata Kitambulisho Cha Taifa Nchini

Na Felix Mwagara, (MOHA), MARA.

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amewataka Watanzania ambao hawajajiandikisha waende kujiandikisha ili waweze kupata kitambulisho cha taifa kwakuwa sio jambo la hiari bali ni lazima kwa kila Tanzania aliyeko ndani ya mipaka ya nchi kutambuliwa.

Akizungumza na wananchi wa Kata ya Nansimo, Mwibara, Wilaya ya Bunda, Mkoani Mara, Lugola amesema katika Mkoa na mikoa mingineyo zoezi la kujiandikisha lilishakamilika ila wale ambao hawakuandikishwa kipindi kile ambacho Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) wanaandikisha wananchi mitaani, wanapaswa kwenda katika ofisi Wilaya za Mamlaka hiyo ili waweze kujiandikisha.

“Wapo ambao kipindi kile NIDA wanaandikisha wananchi mitaani hawakuwepo hilo nalijua, na pia kuna wale ambao kipindi kile zoezi la kuandikishwa linafanyika walikua hawajafikisha miaka 18, hao wote ambao hawajaandikishwa wanapaswa sasa kwenda kujiandikisha haraka iwezekanavyo katika ofisi za NIDA katika Wilaya zao,” alisema Lugola.

Lug... Continue reading ->Source: Mwanaharakati MzalendoRead More