AJALI YA KENTA YAUA MCHEZAJI WA TIMU YA IYUMBU FC NA KUJERUHI 38 WAKIENDA KUCHEZA MCHEZO WA KIRAFIKI NA TIMU YA MGUNGIRA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

AJALI YA KENTA YAUA MCHEZAJI WA TIMU YA IYUMBU FC NA KUJERUHI 38 WAKIENDA KUCHEZA MCHEZO WA KIRAFIKI NA TIMU YA MGUNGIRA

Na Jumbe Ismailly SINGIDA 
MCHEZAJI mmoja wa timu ya soka ya Kijiji cha Iyumbu,tarafa ya Sepuka,wilayani Ikungi,Mkoani Singida,Mussa Kikumbu (20) amepoteza maisha na wengine 38 wamejeruhiwa vibaya baada ya gari aina ya kenta walilokuwa wakisafiria kwenda kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya Kata ta Mgungira kuacha njia na kupinduka.
Wakiongea kwa nyakati tofauti baadhi ya wachezaji na washabiki waliolazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Singida walisema ajali hiyo ilitokea Okt,07,mwaka huu saa tisa za alasiri wakati wakielekea kwenye mchezo wao wa kirafiki na timu ya kata ya Mgungira.
Mmoja wa majeruhi hao Emanueli Peter alisema waliondoka wakiwa watu 38 kwenye gari hilo na walipoanza safari askari mmoja wa kituo cha polisi Iyumbu alisema yeye hatapanda gari bali angekwenda na usafiri wake wa pikipiki.
Alifafanua majeruhi huyo alaiyelazwa katika wodi namba tatu katika Hospitali hiyo kwamba askari huyo alikuwa nyuma ya garai walilopanda akiendesha huku akionesha kila dalili za kuwa amekunywa ... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More