AJIB AFUNGA ‘BONGE LA BAO’ YANGA YAIKANDAMIZA MBAO FC 2-0 TAIFA NA KURUDI JUU LIGI KUU - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

AJIB AFUNGA ‘BONGE LA BAO’ YANGA YAIKANDAMIZA MBAO FC 2-0 TAIFA NA KURUDI JUU LIGI KUU

Na Sada Salmin, DAR ES SALAAM
TIMU ya Yanga SC imejisogeza hadi nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mbao FC ya Mwanza usiku wa leo Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.
Kwa ushindi huo, Yanga SC inafikisha pointi 16 baada ya kucheza mechi sita, sawa na Singida United yenye wastani mdogo wa mabao na mechi tatu zaidi za kucheza - wakizidiwa pointi moja na Mtibwa Sugar wanaoongoza Ligi Kuu kwa pointi zao 17 za mechi tisa.
Mabingwa watetezi, Simba SC wao wapo nafasi ya nne kwa pointi zao 14 baada ya kucheza mechi saba, wakizidiwa pointi moja na Azam FC iliyocheza mechi saba pia.
Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Hans Mabena wa Tanga aliyesaidiwa na Jesse Erasmo na Makame Mdogo, hadi mapumziko Yanga SC walikuwa mbele kwa bao 1-0.Bao hilo lilifungwa na kiungo Raphael Daudi Alpha dakika ya 16 kwa kichwa akimalizia mpira wa adhabu uliopigwa na kiungo Ibrahim Ajib kutoka upande wa kulia wa Uwanja.
Kipa Beno Kakolanya alifanya kazi nz... Continue reading ->

Source: Bin ZuberyRead More