AJIB ASETI MABAO MAWILI NA KUFUNGA MOJA ZURI YANGA IKIISHINDILIA 3-0 ALLIANCE FC TAIFA - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

AJIB ASETI MABAO MAWILI NA KUFUNGA MOJA ZURI YANGA IKIISHINDILIA 3-0 ALLIANCE FC TAIFA

Na Sada Salmin, DAR ES SALAAM
KIKOSI cha Yanga SC kimeendelea kuwapa faraja mashabiki wake baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Alliance FC jioni ya leo Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.
Kwa ushindi huo uliotokana na mabao ya mshambuliaji Mkongo, Heritier Makambo na wazalendo Mrisho Ngassa na Ibrahim Ajib, Yanga SC inafikisha pointi 19 baada ya kucheza mechi saba, sasa wakipanda nafasi ya pili nyuma ya Azam FC yenye pointi 21 za mechi tisa.
Yanga SC wanawazidi kwa pointi tano mabingwa watetezi, SImba SC wenye pointi 14 za mechi saba, nyuma ya Singida United yenye pointi 17 za mechi 10.
Mkongo, Makambo aliye katika msimu wake wa kwanza tu Yanga SC alianza kufunga bao la kwanza dakika ya 18 akimalizia kwa kichwa krosi ya Ibrahim Ajib aliyepasiwa na mshambuliaji Mrundi, Amissi Tambwe.

Kiungo mshambuliaji, Ibrahim Ajib (kushoto) akishangilia na Mkongo Heritier Makambo baada ya kazi nzuri leo

Ajib tena akampa pasi ndefu mkongwe, Mrisho Khalfan Ngasa kuifungia Yanga SC bao la pili dakika ya 2... Continue reading ->Source: Bin ZuberyRead More