Akaunti rasmi za Facebook na Twitter za rais Uhuru Kenyatta zafutwa, yadaiwa ujumbe tata uliyoandikwa asubuhi ya leo ndiyo chanzo - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Akaunti rasmi za Facebook na Twitter za rais Uhuru Kenyatta zafutwa, yadaiwa ujumbe tata uliyoandikwa asubuhi ya leo ndiyo chanzo

Akaunti zote rasmi za mitandao ya kijamiii ya rais wa Kenya Uhuru Kenyata zimefungwa baada ya kutumiwa na watu ambao ”hawajaidhinishwa”, amesema mkuu wa wafanyakazi wake kwenye ujumbe wa Twitter.

Kwa mujibu wa shirika la habari la BBC, Nzioka Waita hakutoa taarifa kuhusu namna ya uingiliwaji wa mitandao hiyo ulivyotokea, lakini akaongeza kuwa itarejeshwa tena mtandaoni baada ya kuchukuliwa kwa “hatua za suluhu ya tatizo hilo,”


On account of unauthorized access to the official social media handles of H.E the President of the Republic of Kenya, Uhuru Kenyatta .All official social media handles for the President have been temporarily suspended to allow for the necessary remedial measures to be undertaken.

— Nzioka Waita (@NziokaWaita) March 22, 2019

Akaunti za Twitter na Facebook za Bwana Kenyatta zina mamilioni ya wafuasi.

Gazeti la kibinafsi la The Star nchini humo limeripoti kuwa ujumbe uliotumwa kwenye Twitter unaoangaliwa kama kuwa wenye utata wa kisiasa, uliotumwa... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More