AKINAMAMA WALIOJIFUNGUA 67 PAMOJA NA WATOTO WACHANGA 475 WAMEFARIKI MKOANI PWANI KUTOKANA NA UZAZI KATIKA KIPINDI CHA MWAKA 2018 - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

AKINAMAMA WALIOJIFUNGUA 67 PAMOJA NA WATOTO WACHANGA 475 WAMEFARIKI MKOANI PWANI KUTOKANA NA UZAZI KATIKA KIPINDI CHA MWAKA 2018

NA MWAMVUA MWINYI, PWANI JUMLA ya watoto wachanga 475 wamefariki dunia baada ya akinamama 41,064 kujifungua mkoani Pwani, mwaka 2018 ,hali ambayo inaonyesha idadi ya vifo vitokanavyo na uzazi kimkoa bado ipo juu. Aidha kati ya akinamama hao 41,064 waliojifungua akinamama 67 walifariki dunia kutokana na uzazi. 
Hayo yalisemwa na mganga mkuu wa mkoa wa Pwani, dokta Gunini Kamba wakati mkuu wa mkoa wa Pwani, mhandisi Evarist Ndikilo aliposaini hati ya makubaliano na wakuu wa wilaya ya kampeni ya kuzuia vifo vya uzazi, kampeni ambayo itafanyika kwa miezi 12 nchini. Alisema, vifo vya watoto wachanga na akinamama wanaojifungua hali hairidhishi hivyo kampeni hiyo itasaidia kupunguza idadi hiyo. 
Kamba alisema, lengo hilo linaweza kufikiwa endapo akinamama watafuata maelekezo ya kiafya wanayopatiwa wakati wa uzazi ili waweze kuvuka salama katika kipindi cha uzazi. "Vifo 67 kwa waliojifungua na watoto wachanga 475 ukilinganisha na malengo ya Kitaifa bado hali sio nzuri sana "alisisitiza Kamba. P... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More