AL AHLY YAANZA VYEMA LIGI YA MABINGWA AFRIKA, YAICHAPA VITA 2-0 - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

AL AHLY YAANZA VYEMA LIGI YA MABINGWA AFRIKA, YAICHAPA VITA 2-0

TIMU ya Al Ahly ya Misri imeanza vyema hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya ushindi wa mabao 2-0 AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) jana usiku Uwanja wa Borg El Arab mjini Alexandria.
Ushindi huo uliotokana na mabao ya Nasser Maher dakika ya 65 na Ali Maaloul kwa penalti dakika ya 79, unaifanya Al Ahly ianzie nafasi ya pili kwenye Kundi D, ikizidiwa bao moja la kufunga na Simba SC ya Tanzania ambayo nayo jana ilishinda 3-0 nyumbani dhidi ya JS Saoura ya Algeria.
AS Vita jana ililazimika kucheza pungufu tangu dakika ya 36 baada ya beki wake, Dharles Mondia Kalonji kutolewa kwa kadi nyekundu kufuatia kuonyeshwa kadi ya pili ya njano kwa kucheza rafu, ya kwanza akionyeshwa dakika ya 21.
Simba SC sasa itasafiri kuwafuata AS Vita mjini Kinshasa Januari 19, wakati JS Saoura watakuwa wenyeji wa Ahly Januari 18 nchini Algeria.
Naye mshambuliaji mpya wa Ismailia ya Misri, Mtanzania Yahya Zayd hakuwepo hata benchi jana timu yake hiyo ikichapwa 2-0 na wenyeji, TP Mazemb... Continue reading ->
Source: Bin ZuberyRead More