AL AHLY YAKAMILISHA NUSU FAINALI LIGI YA MABINGWA AFRIKA - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

AL AHLY YAKAMILISHA NUSU FAINALI LIGI YA MABINGWA AFRIKA

MABINGWA wa kihistoria wa Afrika, Al Ahly wamekamiloisha idadi ya timu za Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa baada ya kuitoa Horoya ya Guinea usiku wa Jumamosi.
Hiyo ni baada ya ushindi wa mabao 4-0 katika mchezo wa marudiano uliofanyika Uwanja wa wa Jeshi wa Al Salam mjini Cairo, unaofuatia sare ya 0-0 kwenye mchezo wa kwanza mjini Conakry, Guinea.
Mabao ya Al Ahly yamefungwa na Walid Soliman dakika ya 32, Islam Mohareb dakika ya 53, Salah Mohsen dakika ya 69 na Ahmed Fathy dakika ya 90 na ushei.
Ikumbukwe juzi, Wydad Athletic Club walivuliwa ubingwa wa Afrika baada ya kulazimishwa sare ya 0-0 na ES Setif ya Algeria katika mchezo wa marudiano Uwanja wa Mohamed V mjini Casablanca nchini Morocco.

Kwa matokeo hayo, Setif wanasonga mbele katika Nusu Fainali kwa ushindi wa 1-0 walioupata kwenye mchezo wa kwanza Ijumaa iliyopita Uwanja wa Mei 8, 1945 mjini Setif, siku hiyo, bao hilo pekee lilifungwa na beki Msenegal, Isla Daoudi Diomande.
Mechi nyingine za marudiano za Robo Fainali juzi, Esperance... Continue reading ->


Source: Bin ZuberyRead More