Ali Choki- Afya Yangu Inazidi Kuwa Njema Zaidi - Ghafla TZ | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Ali Choki- Afya Yangu Inazidi Kuwa Njema Zaidi

Msanii mkongwe wa muziki wa dansi nchini kutokea katika bendi Ali Choki amefunguka na kuweka wazi kuwa hivi sasa afya yake inazidi kuimarika zaidi tofauti na siku chache zilizopita.


Siku chache tu zilizopita Ali Choki alikuwa Alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kisukari, mapafu na presha hali iliyopelekea kulazwa hospitali.


Lakini Kwenye mahojiano yake na Risasi Vibes, Choki alisema kwa sasa anaendelea vizuri tofauti na ilivyokuwa mwanzo hivyo Mungu akipenda mwishoni mwa mwezi huu ataendelea na kazi ya muziki katika bendi anayoitumikia kwa sasa ya Super Kamanyola jijini Mwanza.Nina furaha kwani kwa sasa naendelea vizuri, hali yangu inaimarika kila siku, Mungu akipenda mwishoni mwa mwezi huu nitapanda jukwaani kama kawaida kwa ajili ya kuwapagawisha mashabiki wangu“. 


The post Ali Choki- Afya Yangu Inazidi Kuwa Njema Zaidi appeared first on Ghafla!Tanzania.... Continue reading ->


Source: Ghafla TZRead More