Ali Kiba Afungukia Tuhuma Za Kushuka Kimuziki - Ghafla TZ | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Ali Kiba Afungukia Tuhuma Za Kushuka Kimuziki

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Ali Salehe Kiba amefunguka na Kupitia vikali tuhuma zinazoendelea Kwenye mitandao ya kijamii na kusema ameshuka Kimuziki.


Habari za Ali Kiba kushuka kimuziki zilianza kushika kasi Miezi michache baada ya kuachwa wimbo wake wa ‘Mvumo wa radi’ ambao mashabiki zake hawakuupenda Lakini pia baada ya kutoawwimbo siku chache zilizopita uliorudiwa ukiwatoa povu zito mashabiki zake.


Kwenye mahojiano na Bongo 5, Ali Kiba amepingana vikali na kauli hiyo ambapo amesema hajashuka kimuziki hata kidogo:Sijashuka kimuziki ningekuwa nimeshuka basi wasingeniingiza kwenye hizo tuzo zao za Afrimma,halafu mimi sifanyi muziki ajili ya tuzo mimi pesa zangu nafanya kwa kuuza muziki wangu na kufanya Show,kwahiyo tuzo sizitilii maanani sana”.Ali Kiba ameachia wimbo mpya unaoenda kwa jina la ‘Mwambie sina’ ambao uneshika namba moja kwa siku kadhaa Kwenye mtandao wa Youtube na mpaka hivi sasa una Jumla ya watazamaji milioni moja.


The post Ali Kiba Afungukia Tuhuma Za ... Continue reading ->


Source: Ghafla TZRead More