Ali Kiba- Dini Yangu Hainiruhusu Kumposti Marehemu Kwenye Mitandao Ya Kijamii - Ghafla TZ | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Ali Kiba- Dini Yangu Hainiruhusu Kumposti Marehemu Kwenye Mitandao Ya Kijamii

Staa wa Muziki wa Bongo fleva anayefanya vizuri na kibao chake cha ‘Mvumo wa Radi’ Ali Kiba amefunguka na kusema hawezi kuposti marehemu Kwenye mitandao ya kijamii kwani dini yake hairuhusu.


Siku ya jana msanii wa Bongo fleva Sam wa Ukweli aliyejuliakana zaidi kwa nyimbo yake ‘Sina raha’ na ‘Huku kwetu’ alifariki dunia baada ya kusumbuliwa na maradhi ya muda mrefu.


Wasanii mbali mbali walijitokeza kuonyesha masikitiko yao ikiwemo kumposti katika mitandao ya kijamii lakini Ali Kiba hakufanya jambo lili pekee a watu kumjia juu msanii huyo.


Kwenye mahojiano na waandishi wa habari, Ali Kiba anafunguka na kusema sababu pekee iliyompelekea asimposti Sam wa Ukweli ni kwa sababu za kidini ambazo hazimruhusu kumuanika marehemu:Nataka niliweke hili sawa kwa jamii mimi dini yangu hairuhusu kumposti marehemu katika mitandao ya kijamii ndio maana watu huwa hawaoni mimi nikiposti lakini huwa marina salamu za rambi rambi kwa familia na si kwa kujionyesha kwa sababu sio lazima na haturuhusiwi  kufanya vitu kama hivyo lakini leo hii ningependa kusema kweli ndugu na jamaa na mashabiki wa Sam wa Ukweli, Nimeguswa na msiba ambao umetokea jana na Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu Mahala pema peponi Inshallah”. 


The post Ali Kiba- Dini Yangu Hainiruhusu Kumposti Marehemu Kwenye Mitandao Ya Kijamii appeared first on Ghafla!Tanzania.


Source: Ghafla TZRead More