Ali Kiba Kuidhamini Timu Yake Ya Coastal Union Kupitia Mo Faya - Ghafla TZ | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Ali Kiba Kuidhamini Timu Yake Ya Coastal Union Kupitia Mo Faya

Staa wa Muziki wa Bongo fleva anayefanya vyema na ngoma yake ya ‘Mvumo wa Radi’ Ali Kiba ameweka wazi kuwa yeye ndio mdhamini Mkuu wa timu yake ya Coastal Union Kupitia kinywaji chake cha Mo Faya.


Wiki chache zilizopita timu ya Coastal Union ilitangaza kumsaini Ali Kiba katika kikosi hicho na siku chache baadae KIba ametangaza Neema kwa timu hiyo.


Kupitia mahojiano yake na Azam Tv msanii huyo anayetamba na kibao cha Mvumo wa Radi  amesema kuwa ameamua kuidhamini Coastal Union ili kuisaidia kurudi katika ubora wake, kwa hiyo kupitia udhamini huo anaamini utaisaidia kufikia malengo.Nitakuwa mchezaji wa Coastal Union Lakini pia nitakuwa mdhamini Mkuu Kupitia kinywaji changu cha Mo Faya ili watu wakiwa wanakuja kuangalia mpira wawe wananunua na vinywaji vitakavyokuwa vinapatikana uwanjani na kuisapoti Coastal Union”.Ali Kiba alizindua rasmi kinywaji chake cha Mo Faya Miezi michache iliyopita lakini hakijaweza kuingia sokoni mpaka leo kwa sababu ya kuugua kwa Ommy Dimpoz.


The pos... Continue reading ->


Source: Ghafla TZRead More