Ali Kiba- Sifanyi Muziki Ili Kupata Tuzo, Nafanya Muziki Kwajili Ya - Ghafla TZ | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Ali Kiba- Sifanyi Muziki Ili Kupata Tuzo, Nafanya Muziki Kwajili Ya

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Ali salehe Kiba amefunguka na kuweka wazi kuwa anapokuwa anafanya anaangalia zaidi kuwafurahisha mashabiki na sio kupata tuzo.


Kauli hiyo ya Ali Kiba imekuja siku moja baada ya taarifa za kwamba yeye pamoja na wasanii kama Diamond na Wengineo waliokuwa wanawania tuzo za Afrimma kukosa na kuambulia patupu.


Kwa miaka miwili mfululizo Ali Kiba amekuwa akifanya vizuri katika tuzo za Afrimma ambapo hta mwaka jana alimbwaga Msanii mwenzake Diamond Platnumz na kuchukua tuzo.


Kwenye mahojiano na Bongo 5, Ali Kiba amefunguka na kusema hajaumizwa sana na kukosa Tuzo kwani tangu Mwanzoni hakuwa alifanya ili kupata tuzo:


Unajua siku zote kuna kupata na kukosa na pia Tuzo lazima upromote lakini mimi sijawahi hata siku moja kuomba kupigiwa kura kwa sababu sijawahi kuzipa kipaumbele tuzo na pia sifanyi Muziki kwa ajili ya kupata tuzo nia yangu ni kuwafurahisha mashabiki zangu kwa muziki mzuri”.


Lakini pia Kwenye mahojiano hayo Ali Kiba amefunguka na kuweka wazi kuwa... Continue reading ->


Source: Ghafla TZRead More