Alichojibu Nyandu Tozzy Kuhusu Kolabo na Harmonize. - Ghafla TZ | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Alichojibu Nyandu Tozzy Kuhusu Kolabo na Harmonize.

Msanii wa muziki Bongo, Nyandu Tozzy amefunguka kuhusu mipango ya kufanya kolabo na Harmonize.

Nyandu Tozzy ambaye anafanya vizuri na wimbo mpya ‘I don’t care’ amesema kuwa kutokana na ukaribu wao lolote linaweza kutokea lakini bado hawajakaa na kuzungumzia hilo.


Unajua kwanza naweze kusema mimi na Harmonize ni wana ambao hatuwezi kukaa wiki mbili hatujawasiliana, so naweza kusema ni mdogo wangu kwenye huu muziki. Hivyo usishangae chochote kikatoka baina yangu mimi na yeye,” Nyandu ameiambia The Playlist ya Times FM.


Nyandu Tozzy amekuwa akitumbuiza kwenye show kadhaa ambazo Harmonize amekuwa akiziandaa ikiwemo ile aliyofanya Dar Live mwaka huu.


The post Alichojibu Nyandu Tozzy Kuhusu Kolabo na Harmonize. appeared first on Ghafla!Tanzania.


Source: Ghafla TZRead More