Alikiba, Diamond na Wizkid watemwa tuzo za MTV EMA 2018, Afrika Mashariki yatoa msanii mmoja - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Alikiba, Diamond na Wizkid watemwa tuzo za MTV EMA 2018, Afrika Mashariki yatoa msanii mmoja

Kwa mara nyingine tena Tanzania imekosa mwakilishi kwenye tuzo za MTV EMA 2018 wa kuwania kipengele cha Best African Act.Kwa miaka minne nyuma Alikiba na Diamond Platnumz kutoka Tanzania waliwahi kushinda tuzo hiyo kupitia kwenye kipengele cha Best African Act.


Kwenye orodha hiyo ya wasanii watakaochuana kwenye kipengele cha Best African Act ni Davido na Tiwa Savage wote kutoka Nigeria, Distruction Boyz na Shekinah kutoka Afrika Kusini na Fally Ipupa DR Congo.


Mwingine aliyekuwa Nominated ni Nyansiski kutoka Kenya na ndiye mwakilishi pekee kutoka Afrika Mashariki, kipengele hicho mwaka jana kilichukuliwa na Davido.


SOMA ZAIDI – Alikiba akabidhiwa tuzo yake ya MTV EMA


Huu ni mwaka wa tatu mfululizo kwa wasanii kutoka Tanzania kushindwa kutajwa kwenye tuzo hizo kubwa duniani, baada ya kuchukua tuzo hizo mfululizo mwaka 2015 Diamond Platnumz, na 2016 Alikiba.


Unaweza kumpigia kura msanii wako HAPA na kuangalia orodha kamili ya majina ya wasanii wanaowania tuzo za MTV EMA 2018 HAPA... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More