ALIKOTOKA HUSSEIN JUMBE ‘MZEE WA KUCHECHEMEA’ - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

ALIKOTOKA HUSSEIN JUMBE ‘MZEE WA KUCHECHEMEA’


Na Moshy Kiyungi,Dar es Salaam.
Mwanamuziki Hussein Jumbe anayo historia ndefu katika muziki hadi kuweza kumiliki bendi yake.
Wanamuziki wengi hapa nchini wamepitia mitihani mingi, ikiwemo ya taabu, mashaka na vikwazo kemkemu hadi kuyafika mafanikio.
Hapa uvumulivu wa mtu binafsi unachukua nafasi kubwa ya kuyafikia mafanikio hayo wala siyo kukata tamaa.Husseni Suleiman Jumbe 'Mzee wa Dodo' kama anavyojulikana kwa wengi, ni mifano unaoweza kuyakinisha hayo.
Ni mwanamuziki nguli aliyejaaliwa vipaji adhimu vya sauti ya uimbaji, utunzi uliojaa hisia na zinazosisimua zaidi, ambazo mara nyingi hugusa kila rika la watu.Jumbe alipata elimu yake ya msingi katika Shule za Uhuru Mchanganyiko na Sekondari ya Muslim, zote za Dar es Salaam.‘Mzee wa Dodo’ aliwahi kutamka kuwa aliamua kujifunza muziki baada ya kuvutiwa na nyimbo za marehemu Marijani Rajab 'Jabali la muziki'."Nilikuwa natembea na radio yangu kwa ajili ya kusikiliza nyimbo za Marijani, enzi hizo akiwa na bendi ya Safari Trippers,” Jumbe al... Continue reading ->
Source: Issa MichuziRead More