ALIYEKUWA KIPA WA SIMBA SC AFAFRIKI DUNIA BAADA YA KUANGUKA MAZOEZINI JESHINI - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

ALIYEKUWA KIPA WA SIMBA SC AFAFRIKI DUNIA BAADA YA KUANGUKA MAZOEZINI JESHINI

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
ALIYEWAHI kuwa kipa wa Simba SC, kati ya 2012 na 2013, Hamadi Waziri amefariki dunia jana asubuhi baada ya kuanguka mazoezini Uwanja wa Air Winga, Ukonga mjini Dar es Salaam akiwa na timu yake, Transit Camp ya Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara.
Kocha Mkuu wa Transit Camp, Neville Kanza amesema kwamba Waziri amefariki dunia jana baada ya kuanguka mazoezini asubuhi na mwili wake upo hospitali ya Lugalo mjini Dar es Salaam kwa sasa.
“Hamad tulikuwa naye mazoezini jana Uwanja Air Wing katika hali ya mvua mvua, Uwanja ulikuwa una maji maji na sisi tulikuwa tunafanya mazoezi ya kukimbia, sasa kiatu chake kikafunguka kamba akainama kufunga akainuka na kuanza kukimbia tena, kama hatua mbili hivi akadondoka ghafla kwa kishindo,” amesema Kocha Kanza na kuongeza. 
“Alidondokea sehemu ngumu ambayo ilimpasua juu ya paji la uso, akakimbizwa hopsitali ya pale pale Air Wing, baada ya kama saa moja madaktari wakathibitisha amefariki ndipo akahamishiwa hospiali ya L... Continue reading ->
Source: Bin ZuberyRead More