ALIYEKUWA MKURUGENZI TPA NA WENZAKE WAPELEKWA KIZIMBANI KWA MATUMIZI MABAYA YA MADARAKA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

ALIYEKUWA MKURUGENZI TPA NA WENZAKE WAPELEKWA KIZIMBANI KWA MATUMIZI MABAYA YA MADARAKA

Aliyekuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA),  Ephraim Mgawe na wenzake watatu wamefikiwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka matatu likiwemo la matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia serikali hasara ya Sh. milioni 984.8.
Mbali na Mgawe washtakiwa wengine ni, Wajumbe wa Bodi ya Manunuzi ya TPA, Happiness Senkoro, Apolonia Mosha na Theophil Kimaro.
Akisoma hati ya mashtaka wakili wa Serikali Mwandamizi, Patrick Mwita akisaidiana na Wakili wa Takukuru Maghela Ndimbo, amedai, Septemba 28,2010 katika ofisi za TPA zilizopo Ilala jijini Dar es Salaam, washtakiwa walitenda kosa
Mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu,  Wilbard Mashauri. Imedaiwa, siku hiyo mshtakiwa Mgawe akiwa mtumishi wa umma kama Mkurugenzi Mkuu na ofisa masulufu,  alitumia madaraka yake vibaya kwa kushuhudia mikataba kati ya TPA na Kampuni Leighton Offshore Pte Ltd 19800397 na kupata faida ya Sh. 984,828,000 baada ya kuvunja sheria ya manunuzi kwa kuiwezesha kampuni hiyo kupata upendeleo.... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More