ALIYEKUWA RAIS WA MIGODI YA MADINI AFIKISHWA MAHAKAMA YA KISUTU JIJINI DAR LEO - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

ALIYEKUWA RAIS WA MIGODI YA MADINI AFIKISHWA MAHAKAMA YA KISUTU JIJINI DAR LEO

Na Karama Kenyunko, glogu ya jamiiALIYEKUWA Rais wa Migodi ya Pangea, North Mara, exploration na Bulyanhulu, Deogratius Mwanyika na Meneja Mahusiano wa Mgodi wa Bulyanhulu Alex Lugendo leo Oktoba 17.2018 wemefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka 39, yakiwemo ya utakatishaji na kukwepa kodi zaidi ya USD milioni  112.
Washtakiwa wamesomewa mashtaka yao leo mbele ya Hakimu  Mkazi  Mfawidhi,  Kevin Mhina na Jopo la mawakili watatu waliokuwa wakiongozwa na wakili  wa  serikali  Mkuu,  Faraja  Nchimbi  akisaidiana na Wakili wa serikali Mwandamizi,  Shadrack  Kimaro na Jackilline Nyantori.
Mbali na Mwanyika na Lugendo, washtakiwa wengine ni kampuni ya Mgodi ya Pangea, North Mara, Exploration na Bulyanhulu.
Washtakiwa wanakabiliwa na mashtaka ya kula njama 3, mashtaka yavkughushi 7.

Utakatishaji wa fedha 17, Kuwasilisha nyaraka  za uongo  kwa  Mamlaka ya Mapato Tanzanian (TRA), shtaka moja, kuongoza uhalifu wa kupangwa shtaka moja, kukwepa kodi, ma... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More