ALIYEWAHI KUWA MKUU WA WIILAYA MBALIMBALI AFARIKI DUNIA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

ALIYEWAHI KUWA MKUU WA WIILAYA MBALIMBALI AFARIKI DUNIA

ALIYEWAHI kuwa mkuu wa wilaya tofauti hapa nchini wakati wa serikali ya awamu ya kwanza na baadaye kushika nyadhifa mbalimbali serikalini ,Waziri Juma Waziri amefariki dunia akitibiwa hospitali ya Hindu Mandal jijini Dar es salaam Juzi na anatarajiwa kuzikwa leo nyumbani kwao Sungwi baada ya swala adhuhuri.

Kwa mujibu wa watu wa karibu na mzee Waziri, msiba upo nyumbani kwake Tandika Berege Nyumba namba tatu.Mzee Waziri ambaye mwaka huu anatimiza miaka 89 alikufa siku chache tu baada ya kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa.Akiwa amehudumu katika wilaya mbalimbali zikiwamo Ngara, Pangani , Morogoro, Dodoma, Singida ni mmoja wa watumishi wa serikali waliofanyakazi kubwa ya kupambana na Nyarubanja, mfumo wa umiliki uliokuwa ukiendeshwa Mkoa wa Ziwa Magharibi.

Akiwa amesoma shule ya Msingi Pugu na kisha kusoma sekondari ya Minaki ni mmoja wa watanzania wa mwanzo waliokuwa na kazi kubwa ya kuonesha njia katika siasa za ujamaa na kujitegemea wakifuata maelekezo ya mwalimu.Katika m... Continue reading ->
Source: Issa MichuziRead More