ALLIANCE FC NA BIASHARA UNITED ZAFIKISHA MECHI TATU KILA TIMU BILA USHINDI LIGI KUU - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

ALLIANCE FC NA BIASHARA UNITED ZAFIKISHA MECHI TATU KILA TIMU BILA USHINDI LIGI KUU

Na Mwandishi Wetu, MWANZA
TIMU ya Alliance FC leo imeshindwa kutumia vizuri fursa ya kucheza nyumbani baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 na Biashara United ya Musoma mkoani Mara Uwanja wa Nyamagana mjini Mwanza.
Mshambuliaji mkongwe wa kimataifa wa Tanzania, Jerson John Tegete alianza kuwafungia Alliance FC dakika ya 11, akimalizia pasi ya Sameer Vincent, kabla ya  Innocent Edwin kuwasawazishia Biashara United dakika ya  45.
Huo unakuwa mchezo wa tatu mfululizo kwa kila timu kucheza bila ushindi, Alliance wakitoa sare ya 1-1 na Mbao FC kabla ya kufungwa na Kagera Sugar 2-1 mjini Mwanza.

Nao Biashara United waliuanza msimu kwa kufungwa 2-0 na Kagera Sugar Uwanja wa Karume mjini Musoma kabla ya kuchapwa 1-0 na Mbao FC Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza. 
Ligi Kuu ya Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea kesho kwa mechi tano kuchezwa kwenye viwanja tofauti nchini.
Namungo FC na Mwadui FC Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi, JKT Tanzania na Mtibwa Sugar Uwanja wa Meja Isamuhyo huko Mbweni, ... Continue reading ->Source: Bin ZuberyRead More