Alliance Fc”Tupo Iringa tunasaka madini ya kuwabomoa matajiri wa Mbeya City” - Shaffih Dauda | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Alliance Fc”Tupo Iringa tunasaka madini ya kuwabomoa matajiri wa Mbeya City”

Baada ya matokeo hafifu klabu ya Alliance kupitia msemaji wake Mwafulango Lucas wameelezea maandalizi yao ya mchezo unaokuja dhidi ya mbeya City.


“Tuko mkoani Iringa, tukiendelea na maandalizi ya kucheza mchezo wetu unaofata wa ligi Kuu Tanzania bara dhidi ya timu ya soka ya Mbeya city”


Ratiba za mtanange huo


Mchezo utakaochezwa kwanzia majira ya saa nane kamili za mchana siku ya Jumapili ndani ya uwanja wa Sokoine.


Benchi la ufundi la lipoje?


“Bado tuna imani na benchi la ufundi chini ya kocha mkuu Ramagata Mkungwa Renatus Shija, Chris Brown Mzirai, Daktari wa timu Mzee Ahabed Shindika. Bila kumsahau Josephat Munge, na benchi zima la ufundi kama nilivyosema”Licha klabu hiyo kupata matokeo mabaya msemaji huyo amezidi kuwatia hamasa mashabiki na wadau wa soka kuwa bado klabu yao ipo sawa.


“Tuna imani kubwa na wachezaji wetu. Nasi kama uongozi tumejipanga ndio maana tumeamua kwa dhati timu kubaki mkoani Iringa tayari kujiandaa na mchezo wenyewe”


Kwanini mpaka sasa wapo mkoani Iringa? Je kuma siri gani kubwa?,


“Tunafahamu hali ya hewa ya mkoa wa Iringa na Mbeya inaendena kwa kila kitu. Kwaiyo tunajiandaa kikamilifu kuelekea mchezo huo”


Kocha mkuu wa klabu nae ana yapi?


“kocha anaendelea kuweka mbinu zake, anaweka madini yake kuelekea mchezo huo, na tunaamini vijana watayashika mafunzo ya mwalimu kwa ufasaha”


Vipi kuhusu safari yao kwenda Jijinj Mbeya?


“Timu itaondoka hapa siku ya Jumamosi asubuhi kabisa kuwahi mkoani Mbeya, ama jijini Mbeya kuwahi kuwavaa matajiri wa jiji Jumapili”


Je kuna taarifa zozote za majeruhi? Vipi hali ya kipa wao tegemezi?


“Kiuhalisia kikosi chetu hakina majeruhi wengi. Mchezaji ambaye anaweza kuukosa mchezo huo kutokana na hali ya majeruhi. Golikipa Kelvin Richard aliyekuwa majeruhi, ameanza mazoezi hivi sasa, na daktari wa timu amethibitisha Mwalimu anaweza kumtumia katika mchezo unaofata, itakuwa jukumu la Mwalimu kumtumia au kutomtumia”


Wanaonaje hali ya wachezaji wao kimchezo ba kisaikolojia?


“Wachezaji wetu wako fiti kuivaa timu ya soka ya Mbeya city siku ya tarehe 16, na tuna uhitaji mkubwa wa alama tatu”


Wao wana mtazamo gani kwa wapinzani wao?


“Tunafahamu Mbeya city walipoteza michezo yao mitatu, na sisi tumepoteza michezo miwili tukitoka sare mchezo mmoja”“Tunafahamu kila timu inaingia uwanjani ikitafuta matokeo katika mchezo huo. Lakini tunaamini timu iliyojiandaa vizuri itaweza kucheza vizuri katika mchezo unaofata”


Neno lao kwa mashabiki wao wa mkoa wa mwanza na popote pale?


“Kikubwa niwatoe hofu mashabiki wa Alliance football klabu, popote walipo kwamba timu yao inaendelea vizuri na tunaendlea kujiimarisha vizuri katika kila idara kuelekea mchezo huo. Tuwaombe tu waendelee kutusupoti, waendelee kutuombea”


Mikakati mingine ya timu kwa sasa?


“Kama utaratibu niliokuwa nimejiwekea, kwamba kocha mkuu, na nahodha mkuu mtamsikia siku ya Ijumaa mapema kabisa ntawatupieni taarifa yao wakizungumza kuelekea mchezo wenyewe siku ya Jumapili.Ratiba za mazoezi yapoje?


“Kwasasa tunamuacha Mwalimu na wachezaji wake kuendelea kuendeleza programu zao. Timu ikifanya mazoezi mara mbili kwa siku. Asubuhi na jioni. Na inafanya mazoezi kwa kuelekea mchezo wenyewe wa Jumapili. Kwaiyo ningependa niwajulishe tu kinachoendelea katika kambi yetu ya Alliance football klabu, kwamba hali ni shwari, hali iko vizuri, wachezaji wana morali, wana shauku kubwa, wana hamasa kubwa, wana kimuhemuhe kikubwa kuelekea mchezo huo.


Pia wanazidi kuwakumbusha mashabiki wao kwamba?


“Ni maombi yenu, sala zenu, hasa nyinyi mashabiki wa Alliance football klabu. Na sisi pia tunajiombea na kuendelea kuomba kila siku. Hata wenzetu pia wanaomba. Lakini yule ambaye ameomba vizuri na kujiandaa vizuri anaweza kupata matokeo siku ya Jumapili. Kwaiyo nitangulize kusema kwamba, tutaendelea kupambana ili tutoke sehemu tuliyopo. Tunaamini tupo sehemu ambayo si nzuri na ndomaana tunaendelea kupambana.”


Majina yangu ni Luka Mwaflango wa idara ya habari ya mawasiliano ya Alliance football club.
Source: Shaffih DaudaRead More