ALLIANCE FC YAENDELEZA WIMBI LA USHINDI MECHI ZA KUJIANDAA NA MSIMU, YAICHAPA NA SINGIDA UNITED 2-1 - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

ALLIANCE FC YAENDELEZA WIMBI LA USHINDI MECHI ZA KUJIANDAA NA MSIMU, YAICHAPA NA SINGIDA UNITED 2-1

Na Mwandishi Wetu, MWANZA
TIMU ya Alliance FC leo imeiadhibu Singida United baada ya kuichapa mabao 2-1 katika mchezo wa Kombe la Lake Zone PreSeason 2018 Uwanja wa Nyamagana mjini Mwanza.
Mabaonya Alliance FC katika mchezo wa leo yamefungwa na Israel Patrick dakika ya tano na Maganda Mchembe dakika ya 39 wakati la Singida United limefungwa na John Tiber dakika ya 85.
Huo unakuwa ushindi wa tatu mfululizo katika mechi zake za kujiandaa na msimu ujao wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, baada ya Alliance FC inayofundishwa na Kocha Mkuu, Mbwana Makatta kushinda 4-0 dhidi ya GIPCO ya Geita na 2-1 dhidi ya Kagera Sugar.

Alliance FC ambayo kwa misimu miwili iliyopita imekuwa ikiikosakosa nafasi ya kupanda Ligi Kuu, hatimaye msimu huu imeitimiza ndoto zake na watakuwa miongoni mwa timu 20 zitakazocheza ligi hiyo.
Ligi Kuu inatarajiwa kuanza Agosti 22 na Alliance watafungua dimba na mahasimu wao wa Jiji, Mbao FC Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza, huku Ruvu Shooting ikimenyana na Ndanda FC ya Mtwara Uwan... Continue reading ->


Source: Bin ZuberyRead More