ALLIANCE FC YALAZIMISHWA SARE NA TANZANIA PRISONS, ZATOKA 1-1 NYAMAGANA - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

ALLIANCE FC YALAZIMISHWA SARE NA TANZANIA PRISONS, ZATOKA 1-1 NYAMAGANA

Na Mwandishi Wetu, MWANZA
TIMU ya Alliance FC imelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Tanzania Prisons katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania jioni ya leo Uwanja wa Nyamagana mjini Mwanza.
Na pongezi kwa mshambuliaji mkongwe, Hussein Javu aliyewika klabu za Mtibwa Sugar ya Morogoro na Yanga SC ya Dar es Salaam aliyeifungia Alliance bao la kusawazisha dakika ya 42.
Javu anayecheza kwa mkopo Alliance FC kutoka Mtibwa Sugar, alifunga bao hilo baada ya Michael Ismail kuanza kuwafungia Tanzania Prisons dakika ya 16.
Matokeo hayo yanayoiongezea kila timu pointi moja, yanaifanya Alliance FC ifikishe pointi 25 baada ya kucheza mechi 22 na kupanda hadi nafasi ya 11 kutoka ya 14, wakati Tanzania Prisons inafikisha pointi 16 baada ya kucheza mechi 21 na kupanda kwa nafasi moja hadi ya 19 kwenye ligi ya timu 20.

Mchezo mwingine wa Ligi Kuu unafuatia hivi sasa kati ya wenyeji, Yanga SC dhidi ya Mwadui FC Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.  
Yanga SC ndiyo inaongoza Ligi Kuu kwa sasa ikiwa na pointi... Continue reading ->Source: Bin ZuberyRead More