ALLIANCE WAIPIGA MTIBWA 1-0 NYAMAGANA, MWADUI FC WAITAFUNA LIPULI, NDANDA WAMELAMBWA NA COASTAL - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

ALLIANCE WAIPIGA MTIBWA 1-0 NYAMAGANA, MWADUI FC WAITAFUNA LIPULI, NDANDA WAMELAMBWA NA COASTAL

Na Mwandishi Wetu, MWANZA
TIMU ya Alliance FC imeendelea kukunjua makucha baada ya leo kupata ushindi wake wa tatu wa msimu katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara kufuatia kuilaza 1-0 Mtibwa Sugar ya Morogoro Uwanja wa Nyamagana mjini Mwanza.
Shujaa wa Alliance FC leo amekuwa ni mshambuliaji wake mahiri, Dickson Ambundo aliyefunga bao hilo pekee dakika ya 54.
Kwa ushindi huo, Alliance FC inafikisha pointi 13 baada ya kuchezesha 14 ikipanda kwa nafasi tatu hadi ya 16, wakati Mtibwa Sugar inaendelea kushika nafasi ya nne kwa pointi zake 23 za mechi 14, ikiwa nyuma ya Azam FC pointi 30 mechi 12, Simba SC pointi 26 mechi 11 na Yanga SC pointi 26 mechi 10.
Mechi nyingine za Ligi Kuu leo, bao pekee la Jean- Marie Girukwishaka kwa penalti dakika ya 29, limetosha kuipa Mwadui FC ushindi wa 1-0 dhidi ya Lipuli FC ya Iringa Uwanja wa Mwadui Complex wilayani Kishapu mkoani Shinyanga.
Alliance FC leo wameshinda mechi ya tatu ya msimu katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara 

Na Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga, bao p... Continue reading ->


Source: Bin ZuberyRead More