ALLIANCE YAIWEKA PABAYA BIASHARA UNITED, MBEYA CITY YAIUA COASTAL DAKIKA YA MWISHO - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

ALLIANCE YAIWEKA PABAYA BIASHARA UNITED, MBEYA CITY YAIUA COASTAL DAKIKA YA MWISHO

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
TIMU ya Alliance FC ya Mwanza jana imewaadhibu wapinzani wao wa Kanda ya Ziwa, Biashara United kwa kuwachapa 2-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Karume mjini Musoma mkoani Mara.
Mabao ya Alliance FC yalifungwa na mkongwe, mshambuliaji wa zamani wa Yanga SC ya dar es Salaam na Mtibwa Sugar ya Morogoro, Hussein Javu dakika ya saba na Mnigeria Michael Chinedu dakika ya 71, wakati la Biashara United limefungwa na Tariq Kiakala dakika ya 22.
Kwa ushindi huo, Alliance FC inafikisha pointi 44 baada ya kucheza mechi 36 na kujiinua kutoka nafasi ya 15 hadi ya 10, wakati Biashara United inayobaki na pointi zake 40 baada ya kucheza mechi 35 inabaki nafasi ya 18 kwenye ligi ya timu 20. 

Katika mchezo mwingine wa Ligi Kuu jana, bao pekee la Iddi Suleiman ‘Naldo’ dakika ya 90 na ushei liliipa ushindi wa 1-0 Mbeya City dhidi ya Coastal Union ya Tanga Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
Kwa matokeo hayo, Mbeya City inafikisha pointi 46 katika mchezo wa ... Continue reading ->


Source: Bin ZuberyRead More