Amri Said apewa jukumu maalum Mbao FC - Shaffih Dauda | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Amri Said apewa jukumu maalum Mbao FC

Mwenyekiti wa klabu ya Mbao FC ya jijini Mwanza Solly Njashi amesema wamempa jukumu maalum kocha wa timu hiyo Amri Said ambaye ameanza kuifundisha timu hiyo kuanzia msimu huu.


Amri Said ameambiwa ahakikishe Mbao inafika nusu fainali ya kombe la shirikisho la mpira wa miguu Tanzania bara (TFF) au maarufu kwa jina la Azam Sports Federation Cup pamoja na timu kubaki katika nafasi 5 za juu baada ya msimu kumalizika au isitoke ndani ya 10 bora.


“Kila kocha tunamwambia kile tunachokitaka na matarajio ya Mbao. Tulikuwa na mpango kazi wa miaka 5 lakini katika mwaka wa kwanza tukiwa na kocha Etiene lengo la la kwanza ilikuwa ni kucheza robo fainali ya FA na kuibakiza timu ligi kuu matokeo yake tukafika fainali ya FA na tukabaki ligi kuu”-Solly Njashi, mwenyekiti Mbao FC.


“Mwaka uliopita kwenye FA tulitolewa mapema hata robo fainali hatukufika lakini pia tukabaki ligi kuu tukiwa katika nafasi mbaya baada ya kunusurika kushuka daraja.”


“Malengo yetu tumeshamwambia mwalimu (Amri Said kul... Continue reading ->


Source: Shaffih DaudaRead More