AMRI SAID ‘STAM’ AELEZEA MIKAKATI YAKE MBAO FC LIGI KUU MSIMU UJAO - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

AMRI SAID ‘STAM’ AELEZEA MIKAKATI YAKE MBAO FC LIGI KUU MSIMU UJAO

Na Mwandishi Wetu, MWANZA
KOCHA wa Mbao FC, Amri Said ‘Stam’ amesema kwamba lengo lake ni kuifanya Mbao FC imalize ndani ya timu 10 za juu kwenye msimu ujao wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara.
Akizungumza mjini hapa, Amri amesema kwamba  kwa misimu yote miwili iliyopita, Mbao FC ilikuwa inapigania kuepuka kushuka daraja dakika za mwishoni, lakini msimu huu anataka kubadilisha mambo.
“Kuzungunzia ubingwa au kumaliza ndani ya tatu bora, huko parefu, mpira wa Tanzania una mambo mengi sana, lakini kujihakikishia kumaliza ndani ya timu 10 za juu hilo ndilo langu,”amesema.
Amri amesema maandalizi yake kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu yanaendelea vizuri na vijana wake wana hamu kubwa ya kucheza.

Amri Said ‘Stam’ amesema lengo lake ni kuifanya Mbao FC imalize ndani ya timu 10 za juu 

“Najivunia kuwa na aina ya vijana wenye kiu, wenye njaa ya mafanikio ambao wanataka kucheza kuonekana na kuonyesha uwezo wao ili wapate mafanikio,”amesema Amri.
Beki huyo wa zamani wa Simba SC, amejiunga na Mb... Continue reading ->
Source: Bin ZuberyRead More