AMUNIKE KUKUTANA NA MAKOCHA WOTE WA LIGI KUU KUJADILIANA NAO KUHUSU TIMU YA TAIFA - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

AMUNIKE KUKUTANA NA MAKOCHA WOTE WA LIGI KUU KUJADILIANA NAO KUHUSU TIMU YA TAIFA

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
KOCHA mpya Mkuu wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Emmanuel Amunike atakutana na makocha wote wa klabu za Ligi Kuu kujadiliana juu ya masuala ya kiufundi.
Hayo yamesemwa na Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia katika mahojiano maalum na Bin Zubeiry Sports – Online juzi mjini Dar es Salaam.
Karia amesema kwamba mwalimu anataka kukutana na makocha wa klabu za Ligi Kuu ili kujadiliana nao juu ya masuala ya kiufundi kwa manufaa ya timu ya taifa.
“Mwalimu atakutana na makocha wote wa timu za Ligi Kuu, lakini pia atakutana na makocha wa timu za taifa na makocha ambao walikwishafundisha timu za taifa, atakuwa na mazungumzo nao ya kiufundi, baada ya hapo tutakaa ataelekeza Kamati ya Ufundi, utaratibu gani ambao upo,” amesema Karia.

Emmanuel Amunike atakutana na makocha wote wa klabu za Ligi Kuu

Amunike mwenye umri wa miaka 47, amesaini mkataba wa miaka miwili kufundisha Taifa Stars akichukua nafasi ya kocha mzalendo, Salum Ma... Continue reading ->Source: Bin ZuberyRead More