Antony Joshua amchakaza Povetkin kwa TKO, na huu ndio mkwanja aliyoingiza (+video) - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Antony Joshua amchakaza Povetkin kwa TKO, na huu ndio mkwanja aliyoingiza (+video)

Bondia Mrusi Alexander Povetkin amejikuta akishindwa kuvumilia makonde mazito ya Muingereza Anthony Joshua baada ya kukubali kipigo cha TKO katika raundi ya 7 ya pambano lao kali la ubingwa wa dunia uzito wa juu.


Antony Joshua

Povetkin akionekana ni hatari kunako raundi ya kwanza alirusha konde kali lililomtoa Joshua damu puani. Jambo ambalo lilizua hofu kwa mashabiki wa bondia huyo waliohudhuria kwenye pambano  hilo kunako dimba la Wembley .


Hata hivyo, Joshua baadae akaendelea kujilinda zaidi hadi raundi ya 7 alipofanikiwa kumpiga TKO na kunyanyua mkanda wa ubingwa wa dunia wa uzito wajuu.


Kwa ushindi huo, Joshua amefanikiwa kuchukua kiasi cha £uro milioni 20 sawa na Bilioni 54 za Kitanzania huku mwenzie akichukua Euro Milioni 6.


The post Antony Joshua amchakaza Povetkin kwa TKO, na huu ndio mkwanja aliyoingiza (+video) appeared first on Bongo5.com.... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More