Arsenal mikononi mwa Sporting CP usiku wa EUROPA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Arsenal mikononi mwa Sporting CP usiku wa EUROPA

Katika mechi ya nne ya hatua ya makundi kwenye ligi ya EUROPA Alhamisi hii timu ya Arsenal itakuwa nyumbani katika dimba la Emirates dhidi ya Sporting CP ya Ureno. Katika mchezo wao wa mzunguko wa kwanza Arsenal waliibuka na ushindi wa bao 1 ambao uliwawezesha kuwa vinara na kuongoza kundi E.Arsenal wamekuwa katika kiwango bora na wanacheza kandanda safi tangu wampate kocha Unai Emery ambaye amebadilisha aina ya uchezeji wake. Mchezo huo utachezwa Alhamisi tar 8 Novemba, majira ya saa 5:00 Usiku saa za Afrika Mashariki na utarushwa moja kwa moja kupitia chaneli ya ST World Football katika king’amuzi cha StarTimes.Katika Usiku huo wa EUROPA mechi nyingine zitakazochezwa ni pamoja na ule wa Chelsea ambao watakuwa ugenini dhidi ya BATE Borisov (saa 2:55 Usiku), Fenerbahce vs Anderlecht (saa 12:50 jioni), Lazio vs Olympique Marseille (saa 2:55 Usiku), Celtic vs RB Leipzig (saa 5:00 Usiku) na Real Betis vs AC Milan (saa 5:00 Usiku), yote kupitia chaneli za michezo za StarTimes.Michuano ya... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More