ASASI ZA KIRAIA ZAOMBWA KUSHIRIKIANA NA WANANCHI KUTATUA CHANGAMOTO MBALIMBALI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

ASASI ZA KIRAIA ZAOMBWA KUSHIRIKIANA NA WANANCHI KUTATUA CHANGAMOTO MBALIMBALI

Asasi za kiraia zimeombwa kushirikiana na wananchi katika kutatua changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa upatikanaji wa huduma ya maji. 
Diwani wa Kata ya Kwembe wilayani Ubungo, Dweza Kolimba amesema asasi za kiraia zina nafasi kubwa ya kuleta maendeleo katika jamii kwa kushirikiana na wananchi na watendaji wa serikali. 
Akizungumza katika semina iliyoandaliwa na asasi ya Pakacha kwa ajili ya kujadili utatuzi wa changamoto ya maji, kuanzia ufuatiliaji wa rasilimali fedha na utekelezaji wake, Kolimba amesema upatikanaji wa maji katika kata yake umekuwa wa shida, hivyo kupitia asasi kama ya Pakacha, wananchi wanaweza kuelimishwa kushirikiana na viongozi ili kutatua kero hizo. 
Amesema upatikanaji wa maji umekuwa wa shida katika kata yake, huku akisema kuwa wananchi wengi watapata maji baada ya mradi mkubwa wa Luguruni kukamilika. “Tayari mabomba yamesambazwa, hivyo tunaomba mradi huu uishe mapema ili watu wapate maji,” amesema Kolimba. Everyline Francis, mjumbe wa kamati ya maji y... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More