ASEMAVYO EDO KUMWEMBE KUHUSU TIMU YA YANGA - Kajunason | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

ASEMAVYO EDO KUMWEMBE KUHUSU TIMU YA YANGA

Na Edo Kumwembe
USISHANGAE sana Yanga kuwa kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu huku wachezaji wakiwa hawana mishahara. Wana kauli yao inasema ‘Daima mbele nyuma mwiko’. Wakati mwingine Yanga inanikosha sana nje ya uwanja.
Unajua kwanini ipo kileleni huku wachezaji wakiwa hawana mishahara? Sijui hizi timu kubwa zilijiunda vipi wakati huo zikiundwa. Lakini Yanga ni timu ya wananchi. Mashabiki wake ni raia wa kawaida kabisa. Wengi wengi kati yao ni walalahoi na wanaipenda timu yao kupindukia.
Mapenzi yao yanatoa presha kubwa kwa wachezaji. Popote wanapokwenda, hata kama timu yao inapitia kipindi kibovu, Yanga itapokewa na maelfu ya mashabiki huku wengi kati yao wakiwa ni walalahoi. Hapo hapo wachezaji wanapata ari ya kupambana.
Juzi nimeona wametua Mbeya, mashabiki wakajipanga katika mistari miwili kuipokea timu yao. Nilicheka sana nikakumbuka tabia za Yanga. Hilo limetokea wakati timu haina fedha. Hiyo ni janja ya mashabiki kuwatia morali wachezaji. Mbona wakati wana pesa hawajawahi kuwapok... Continue reading ->


Source: KajunasonRead More