ASILIMIA 80 YA WANANCHI SIMIYU KUTUMIA BIMA YA AFYA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

ASILIMIA 80 YA WANANCHI SIMIYU KUTUMIA BIMA YA AFYA

Na Stella Kalinga, Simiyu
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema mkoa huo umejiwekea malengo ya kuhakikisha zaidi ya asilimia 80 ya wananchi wake kuwa na kadi za bima ya afya ili kujihakikishia upatikanaji wa huduma za matibabu katika vituo vya kutolea huduma za afya hapa nchini.
Mtaka ameyasema hayo wakati ufunguzi wa Jukwaa la Ushirika Afya Mkoa wa Simiyu lililofanyika kwa lengo la kujadili namna wanachama wa Vyama vya Ushirika vya Msingi (AMCOS)wanavyoweza kujiunga na Bima ya afya na kupewa kadi kupitia vyama vyao na kama familia, ambalo limefanyika Machi 14, mjini Bariadi.
Amesema yeye kama Mkuu wa Mkoa atafanya vikao na wanachama wa AMCOS na makundi mbalimbali ya wananchi katika wilaya zote mkoani hapa na kuzungumza nao kuwaelimisha juu ya umuhimu wa kila mwananchi kuwa na Bima ya Afya kwa ajili ya matibabu.
Aidha, amesema atawaelimisha wananchi juu ya umuhimu wa kuwa katika Vyama vya Ushirika Vya Msingi ambavyo vinawapa nafasi ya kupata Bima ya afya na kupata matibabu mak... Continue reading ->Source: Issa MichuziRead More