ASILIMIA 86 YA WANAWAKE NA ASILIMIA 100 YA WANAUME WA MKOA WA SHINYANGA WASEMA UMASIKINI NDIO SABABU KUBWA YA MIMBA NA NDOA ZA UTOTONI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

ASILIMIA 86 YA WANAWAKE NA ASILIMIA 100 YA WANAUME WA MKOA WA SHINYANGA WASEMA UMASIKINI NDIO SABABU KUBWA YA MIMBA NA NDOA ZA UTOTONI

Asilimia 86 ya Wanawake na Asilimia 100 ya Wanaume mkoani Shinyanga wanasema kuwa umaskini wa familia ndio chanzo kikubwa cha mimba na ndoa za utotoni.
Hayo yamesemwa na Mwakilishi wa Shirika la Save The Children Bi. Neema Bwaira alipokuwa akitoa mada katika Mdahalo wa Kitaifa unaoendelea jijini Dar es Salaam kuhusu namana bora ya kupambana na ukeketaji, mimba na ndoa za utotoni.
Bi Neema ameongeza kuwa waliamua kufanya utafiti huu mdogo ili kupata kujua uelewa wa jamii ya mkoa wa Shinyanga katika suala la mimba na ndoa za utotoni.
Ameongeza kuwa utafiti huo umefanyika katika Wilaya za Kishapu, Kahama na Shinyanga Mjini ambapo umebaini  kuwa jamii bado haina uelewa kuhusu madhara ya mimba na ndoa za utotoni na bado vitendo hivi vimekumbatiwa kwenye mwamvuli wa mila na desturi.
“Kwa mujibu wa utafiti huu mdogo tulioufanya tumebaini kuwa umasikini na uelewa mdogo wa jamii kuhusu madhara ya mimba na ndoa za utotoni” alisisitiza Bi. Neema.
Bi Neema ameeleza kuwa Asilimia 11 ya wavulana na... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More